Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, December 15, 2009

Simba haitikisiki na mkwala wa TFF

Uongozi wa klabu ya Simba umesema haustushwi na tishio la Shirikisho la Soka nchini (TFF), kwamba hawatashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na kuchelewesha kupeleka majina ya usajili wa wachezaji kwasababu wanaifahamu tarehe ya mwisho ya zoezi hilo kuwa ni leo. TFF ilizitaka klabu za Simba na Yanga, inayoshiriki michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika, kuwakilisha majina ya usajili wa wachezaji wao watakaoshiriki michuano hiyo inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika, CAF, Jumamosi iliyopita, ambapo Yanga ilitekeleza lakini Simba waliomba waongezewe muda wa siku moja ili kukamilisha jambo hilo. TFF iliipa muda huo Simba na kuitaka iwe imekamilisha zoezi hilo juzi Jumapili. Hata hivyo, pamoja na kuongezewa muda huo bado uongozi wa Simba ulishindwa kutekeleza agizo hilo hali iyosababisha Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela kuwataka viongozi hao kutekeleza agizo akisisitiza kuwa watakosa michuano hiyo endapo hawatawasilisha majina hayo. Licha ya tishio hilo kutoka TFF, Simba ilishindwa kuwasilisha majina hayo kwa madai kuwa hailitambui agizo la TFF na kwamba wao wanaangalia tarehe ya mwisho ya kuwasilisha majina iliyowekwa na CAF ambayo ni leo Desemba 15. Akizungumza na vyombo vya habari jana, Afisa Habari wa klabu hiyo, Cliford Ndimbo alisema kuwa wanachojua wao ni kuwa siku ya mwisho ya kuwasilisha majina ya wachezaji wao CAF ni leo na si Jumamosi iliyopita kama ilivyotangazwa na TFF. "Hilo agizo la TFF hatulitambui, tunachokijua ni kuwa mwisho wa kuwasilisha majina CAF ni kesho (leo), sasa hayo masuala mengine sisi hatuyapi nafasi kwa sababu tunafanya kazi kwa taratibu tulizojiwekea," alisema Ndimbo. Hata hivyo, alieleza kuwa jana waliwasilisha majina 27 ya wachezaji wao watakaoshiriki michuano hiyo, ambapo katika orodha ya wachezaji wao wote waliowasajili wamewaacha George Nyanda, Adam Kingwande na Meshack Abel ambao wamesajiliwa African lyon kwa mkopo. Lakini Nipashe ilipomuuliza Mwakalebela kama majina ya wachezsaji wa Simba yamefika, alijibu kwa kifupi kuwa bado hawajayawasilisha kwenye ofisi yake. Kwa upande mwingine Ndimbo alisema kuwa timu yao inatarajia kurejea leo kutoka Zanzibar ilikoeweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Tusker ambapo keshokuitwa wataanza mazoezi chini ya kocha wao Patrick Phiri anayetarajia kurejea leo kutoka mapumzikoni nchini Zambia.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote