
Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola wamepokea na kukubali ombi la Rwanda la kuwa mwanachama wa Jumuiya hiyo.Kutokana na uamuzi huo uliofikiwa jana kabla ya kufungwa kwa mkutano huo, Rwanda sasa inakuwa mwanachama wa 54 wa Jumuiya ya Madola. Rwanda ambayo haikutawaliwa na Uingereza inakuwa nchi ya pili baada ya Msumbiji kujiunga na Jumuiya ya madola ambayo inaundwa na nchi zilizokuwa makoloni ya Uingereza. Rwanda ilitawaliwa na Ubelgiji wakati Msumbiji ilikuwa koloni la Ureno. Tayari sekretarieti ya Jumuiya ya Madola imeshamuarifu Rais Paul Kagame wa Rwanda kuhusiana na nchi yake kukubaliwa kuwa mwanachama.
No comments:
Post a Comment