Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Friday, December 18, 2009

Ajifungua akifanya mazoezi Gym

Elizabeth Poblete, 22, mwanamichezo aliyeiwakilisha Chile kwenye mashindano ya kunyanyua vitu vizito kwenye olimpiki mwaka jana nchini China, amejifungua mtoto ndani ya gym alipokuwa akifanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito.Elizabeth alikuwa hajui kama ana mimba na alijifungua mtoto huyo kwenye gym iliyopo kwenye mji wa Sao Paulo nchini Brazili alikoweka makazi yake.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na tovuti ya habari ya Globo.com, Elizabeth alijifungua mtoto wa kiume ambaye amempa jina la Eric Jose.Akiongelea tukio hilo kocha wake wa gym, Horacio Reis, alisema kuwa alikuwa hajui kama Elizabeth alikuwa na mimba kwani wiki iliyopita aliweza kushiriki na kushinda kwenye mashindano ya kubeba vyuma yaliyofanyika nchini Chile."Mashindano yalimalizika salama na alishinda", alisema kocha wake.Kwa mahesabu ya madaktari, Elizabeth alikuwa na mimba ya miezi sita lakini kutokana na lishe na mazoezi aliyokuwa akifanya, mzunguko wake wa damu za hedhi ulikuwa hauna mpangilio maalumu hivyo kumfanya asigundue kuwa ana mimba.Elizabeth aliiwakilisha Chile kwenye mashindano ya olimpiki yaliyofanyika Beijing, China mwaka jana.Katika miezi ya karibuni, alikuwa kwenye mazoezi makali na lishe ya nguvu ili kuupandisha uzito wake kutoka kilo 75 hadi 85.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote