Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, December 31, 2009

Mwanamke Asakwa Dar kwa Mauaji ya kichanga

Mama mmoja Jijini Dar anasakwa na Jeshi la Polisi baada ya kukisokomeza kichanga chake kwenye mfuko wa rambo na hatimaye kukisababishia kifo. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Liberatus Sabas, amesema mama huyo aliweza kutekeleza unyama wa kumtumbukiza mwanae ndani ya mfuko wa rambo na kisha akaenda kumtupa na hatimaye kumsababishia kifo, ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kujifungua.  kichanga hicho kiligundulika majira ya saa 3:30 usiku na wakazi wa eneo hilo la Temeke, kabla ya kufanya utaratibu wa kuripoti tukio hilo polisi. Hata hivyo, akasema polisi walipofika eneo hilo la tukio, walikuta kichanga hicho tayari kimefariki na mwili wake wakaupeleka katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke. Kamanda Sabas akasema juhudi za kumtafuta mwanamke huyo zinaendelea ili akipatikana aweze kufunguliwa kesi ya kuua.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote